Tuesday, May 10, 2016

Jinsi Ya Kufanya Cd Kuweza Kuifungulia Kompyuta

COMPUTER
Wakati mwingine Kompyuta Inakera.

Inaudhi.

Unaweza kuichapa makofi.

Kompyuta ipo slow sana kiasi kwamba unaweza kutoa machozi.

Lakini si lazima uwe mtaalam wa TEHAMA kuweza kutatua tatizo hili. Kuna sababu chungu nzima kwa nini kompyuta yako ipo slow. Na kwa hakika kama hujui wapi uanze kutatua tatizo hilo, unaweza kujikuta unatamani upate kompyuta mpya.

Mojawapo ya suluhisho la kwa nini kompyuta yako inafanya kazi taratibu – kama vile konokono, ni kujua sababu zinazopelekea hali hiyo. Nina sababu kama 8 hivi ambazo zinaweza kukusaidia kubaini chanzo cha kompyuta yako kuwa slow.

Kama kompyuta yako ina kiwango cha RAM cha kutosha, ni ya kisasa, na haina tatizo lolote la kiufundi, basi soma mambo haya 8 kujua wapi utaanzia kuifanya iwe na kasi kubwa kama mwanzo.
Browser ya intaneti ina rundo la programu

Browser ni program inayokuunganisha wewe katika mtandao wa intaneti. Kuna browsers za aina nyingi lakini nina uhakika hapo ulipo utakuwa unatumia aidha Firefox au Chrome.

Hakikisha browser yako haina program za ziada (zinaitwa plugins kwenye Firefox na Extensions kwenye Chrome). Programu hizi za ziada mara nyingi huwa zinafanya kazi bila wewe kujua (running in the background). Zinatumia rasilimali ya ubongo wa kompyuta pamoja na RAM, sababu ambazo zinaweza kuifanya browser kuwa slow sana.

Artikel Terkait