Tuesday, May 10, 2016

Jinsi Ya Kuomba Na Ubani - Kuswali Swala.

KUSWALI
Asalam Alaykum,
Kuna uhalali/faida/hasara gani wa kutumia ubani kuweka kwenye moto wakati wa kuomba duah au kurehemu ndugu zetu waliotutangulia katika haki?

Wabillah tawfiq

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Swali zuri kuhusu mas-ala hayo. Kufukiza ubani katika moto wakati wa kusoma dua haina uhalali wala faida yoyote.  Na hii imekuwa ni ada ya baadhi ya ndugu zetu hasa wanaosoma Maulidi na Khitma kwa kuamini kuwa du'aa inapanda juu na moshi wake. Yote haya ni mambo ya kijahili yasiyokubalika katika sheria ya Kiislamu.

Inayopatikana ni hasara kubwa kwani ni kwenda kinyume na Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Chetezo cha moto wakati wa ibadah na dua imechukuliwa kutoka kwa Mafursi (Iran) ambao walikuwa wanaabudu jua na moto. Walipoingia katika Uislamu waliingia na baadhi ya desturi zao mbaya zinazokwenda kinyume na Uislamu. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametusisitiza sana tusifuate ada na desturi za makafiri au kujifananisha nao kwani tutakuwa sawa na wao.

Leo pia utakuta wanawake Waislamu wanaoishi India wanavaa sare kama Mabaniyani huku matumbo yao yapo wazi kabisa jambo ambalo linakataliwa na kwenda kinyume na Dini hii ya Kiislamu. Au vijana wa kiume kusuka nywele, kuvaa hereni, mikufu au kuchonga nyusi kwa kuwaiga makafiri wanamuziki na wachezaji mipira, na vijana wa kike kuvaa masuruali kama wanaume n.k.

Na Allah Anajua zaidi

Artikel Terkait