Thursday, June 30, 2016

Jinsi Ja Kuanzisha Kiwanda Cha Chokoleti / Chocolate.

CHOCOLATE
Mambo vipi msomaji wangu natumaini wewe ni mzima wa afya kwa upande wangu namshukuru mungu ni mzima wa afya kabisa

Leo ningependa kukushirikisha ni jinsi gani unaweza kuanzisha kiwanda cha kusindika chakula

Kwa utangulizi tunapaswa kufahamu KIWANDA CHA KUSINDIKA CHAKULA ni kiwanda kinachoshugulika na kuifadhi chakula ili kiweze kudumu kwa muda mrefu zaidi kwaajili ya matumizi mbalimbali

Kuna vitu vya kuzingatia kabla ya kuanzisha kiwanda cha kusindika chakula na kwa kuanza kitu cha kwanza ni upatikanaji wa malighafi  ambazo ni mazao yanayotokana na kilimo au nyama itokanayo na wanyama wa kufugwa au wanyama pori na ni muhimu sana kuanzisha kiwanda hicho karibu na mazingira yatakayo rahisisha upatikanaji wa malighafi husika ili kupunguza gharama za usafirishaji wa malighafi

Pia ni muhimu kuhakikisha una teknolojia ambayo itawezesha kuhifadhi vyakula hivyo hapa tutahusisha kemikali pamoja na nyenzo zitakazo hitajika kuhifadhi vyakula hivyo

Pia ni muhimu kutafuta ushauri kwa wataalamu ili kufanikisha zoezi zima. Na mwisho ni soko la bidhaa hiyo ya chakula ambacho kimesindikwa na bidhaa hiyo inaweza kutumika na mtu yeyote kwaiyo ni muhimu kujenga communications na watu ili kufanikisha upatikanaji wa soko la bidhaa hiyo.

Artikel Terkait