Friday, July 15, 2016

Jinsi Ya Kupata Wawekezaji / Wafadhili.

UJASIRIAMALI
Isaac Oboth ni kijana wa miaka 26 ambaye alianza kuishi kama mtoto yatima akiwa na umri mdoog sana.Alipitia katika maisha ya shida na kushindwa kupatiwa mahitaji yake muhimu katika maisha yake hasa yakiwa ni matokeo ya kukosa wazazi na walezi wa karibu.Hata hivyo katika maisha yake yote,Isaac alikataa kabisa kukata tamaa katika maisha yake.

Kwa leo,Isaac ni mkurugenzi wa kampuni yake aliyoianzisha ya media 256 inayojishughulisha na kurekodi matukio katika video na kutengeneza Makala mbalimbali kwa njia ya video nchini Uganda.Isaac hakuanza kama mtaaalmu wa kurekodi kwa njia ya video,ila anasema safari yake katika kuwa mtaalamu wa video ilianza mwka 2010 kwa tukio lisilo la kawaida.

Wakati akiwa anakaribia kumaliza chuo,waliamua yeye na wenzake kutafuta mtu ambaye angeweza kuja kuwarekodia sherehe yao ya siku ya mahafali wakati wa kumaliza ili kuweka kumbukukumbu nzuri kwa siku zijazo.Hata hivyo baada ya mtu huyo kutengeneza video hiyo,ilionekana kuwa na ubora wa hali ya chini mno ambao ulimchukiza kila mtu.Baada ya kuona hivyo na kusikia kila akilalamika Isaac aliamua kuchukua hatua isiyo ya kawaida katika maisha yake.

Alianza kwenda kwenye internet café iliyokuwa jirani na kaanza kutumia mtandao wa YouTube kujifunza kutoka kwa watu mbalimbali ambao walikuwa wameweka mafunzo yao kuhusu utaalamu wa kurekodi katika mtandao huo.Baada ya muda,Isaac alianza kuwa mtaalamu wa kurekodi kwa njia ya video na alianza kuwaambia watu wampe kazi mbalimbali awafanyie.

Hata hivyo mafanikio makubwa sana ya Isaac yalianza baada ya mwaka mmoja kuona tangazo la CocaCola nchini Uganda na anasema lilifanywa kwa kiwango cha chini sana.Hivyo,alichukua hatua akaenda kuonana na meneja wa Coca-Cola Uganda na akamwambia kuwa anaweza kutengeneza tangazo lenye ubora zaiid ya walilonalo na yuko tayari kulitengeneza na lisipokuwa bora kuliko walilo nalo basi wasimlipe chochote.Baada ya kukubaliwa,alitengeneza tangazo na lilimvutia kila mtu hivyo kkujikuta akipewa mkataba mnono na kampuni ya Coca-Cola.

Baada ya hapo kampuni ya Isaac imeendelea kukua na amefanikiwa kufanya kazi na makampuni na mashirika mbalimbali,ikiwemo UNDP,USAID,Marie Stopes International,African Leadership Academy na Mara Foundation.Kwa sasa kampuni yake imeajiri takribani watu we lakini yeye pia anafundisha katika chuo cha filamu cha Uganda.Kampuni ya Isaac imewahi kuzawadiwa tuzo maalumu ya Anzisha kama mjasiriamali wa mwaka.
Isaac alipoulizwa kuhusu ndoto aliyonayo anasema-“Ni kuifanya kampuni yangu kuwa yenye ubora wa kimataifa.Ni lengo alngu kuiona media 256 ikiwa ni kampuni inayoaminika katika bara lote la Africa na ikishindana na makampuni makubwa ya kutengeneza filamu duniani”

Hakuna mtu aliyezaliwa kuwa na ndoto ndogo,hakuna mtu aliyezaliwa kuwa na maisha ya hali ya chini.Kila mtu ana fursa isiyo na kikomo kufanikiwa katika ndoto na lengo alilonalo maishani.Leo unaposoma Makala hii kumhusu Isaac ningependa kukukumbusha kuwa,wewe ni mtu wa tofauti na ulizaliwa kuleta tofauti katika ulimwengu huu.Bila kujali kama umepitia maisha magumu kama ilivyokuwa uyatima wa Isaac,ni vyema ukajua kuwa historia yako haitakiwi kuwa na nguvu ya kuamua hatima yako.Unayo fursa ya kubadilisha kabisa historia ngumu,yenye maumivu na isiyovutia ambayo uliwahi kuipitia na ukafungua ukurasa mpya wa mafanikio katika maisha yako kuanzia leo.

Isaac hakuwa mtaalamu wa kile anachokifanya leo ila baada ya kugundua kuwa kuna uhitaji aliamua kufanya bidii binafsi kujifunza bila kuchoka.Hakuwa tayari kutumia visingizio vya kukosa walimu au kukosa mafunzo rasmi kumnyime fursa;aliamua kufanya maamuzi yasiyo ya kawaida kutumia masaa mengi katika kujifunza kuhusu jambo jipya alilotaka kulifanya.Katika kile ambacho unataka kukifanya katika maisha yako,ni muhimu sana utumie muda wako kujifunza na kupata maarifa ya kutosha.Tafuta vitabu,majarida na hata tumia mitandao kujifunza kwa kasi.Hebu jiulize,hivi ni asilimia ngapi ya muda wako unaitumia kujifunza kutoka mitandaoni ukilinganisha na asilimia ambazo huwa unaperuzi ili kujifurahisha tu.

Ili utimize ndoot yako lazima ujiamini na lazima uwe tayari kufanya jambo la kujihatarisha(take risk).Ukikosa kujiamini na kuamini uanchokifanya utafanya kila mtu ashidnwe kukuamini kabisa.Kuna watu wanauza bidhaa lakini hawana ujasiir hata wa kuwaambia wengine,kuna watu wanatoa huduma fulani lakini hawana kabisa ujasiir wa kuwaambia watu.Isaac hakusubiri tangazo la tenda litolewe,alichukua hatua ya ujasiri na akaenda kumuona meneja wa Coca-Cola na akaonyesha uwezo wa kile anachokifanya.Sio kila fursa inasubiriwa,kuna fursa zingine unatakiwa uzifuate.Inawezekana umekuwa ukisubiri sana fursa zikujie,ni wakati wa kubadilisha staili sasa na kuanza kuzifuata mara moja.Chukua hatua leo.

Wazo dogo ulilonalo leo ni kampuni kubwa sana ya kesho,mradi mdogo unaotamani kuuanza leo ni kampuni ya kimataifa itakayotikisa Tanzania kesho,wito wa maisha yako uliopewa na Mungu leo utatumika kusaidia mamilioini kesho-Usikate tamaa,Usiishie njiani.

Artikel Terkait