Wednesday, August 17, 2016

Jinsi Ya Kujua Iwapo Mtoto Amegeuka Tumboni.

UJAUZITO
Hongera mama kwa kufikisha miezi 8 (wiki 32) umebakiza mwezi mmoja ujifungue.Mtoto ameshakuwa mkubwa na uzito umeongezeka mama na kuelemewa wakti mwingine ,mabadiliko ya mtoto ni

    Uzito wa mtoto ni 2kg au 2.5g

    Urefu wa mtoto ni inches 16-17
    Kila mtoto alalapo analala kwa muda wa dakika 20-40
    Viungo vya mtoto bado vinaendelea kukua na kukomaa lishe bora ni muhimu kwa mama ili kusupport ukuaji wa mtoto.

    Kichwa kimegeuka na kuangalia chini tayari kusubiri kutoka ,kwa mara nyingi kichwa kitakuwa chini mpaka mda wa kujifungua utakapo fika,japo kuna wakati wanajigeuza na baadhi ya hospital watakusaidia kumgeuza kwani ni hatari mtoto kugeuza kichwa kuangalia juu kwa miezi ya 8-9,iwapo mama akashikwa uchungu mtoto anaweza tanguliza mkono,miguu badala ya kichwa ni ni hatari,mtoto anauwezo wa kujigeuza pia mwenyewe bila msaada wa hospital.
    Mtoto anauwezo wa kusikia sauti za nje za watu wakiongea au music

Mabadiliko ya mama
    Kutanuka kwa njia ya uzazi ,utasikia ukeni panavuta vuta na maumivu ya kuja na kuondoka
    Kupata tabu ya kupumua ,mtoto anakubana sana haswa sehemu ya mbavu na upumuaji wako unakuwa mgumu
    Mafua ya kudumu (sio kwa wote)
    Matiti kuanza kuvuja maziwa
    Kuchoka kwa mama kunaongezeaka
    Kutokwa maji maji ukeni
    Kiungulia (heartburn)
    Maumivu ya mgongo
    Mama anakojoa mara kwa mara
    Tumboni kwa mama utapata mstari mweusi toka juu kuja chini unaitwa Linea nigra
    Kulala kwa tabu usiku

Ushauri
Endelea na mazoezi ya kuogelea,kutembea,stretching ,yoga n.k epuka kubeba vitu vizito,kuruka kamba au kukimbia ni hatari kichwa cha mtoto kinaangalia chini kwa sasa.Mama unaweza fanya shopping ya mtoto ,na kuanza kuapack bag utakalo enda nalo hospital siku ya kujifungua,fatilia posts zijazo utaona list ya vitu unavyotakiwa kubeba.

Ukaona dalili hizi wahi hospital
    kuvimba miguu,mikono,kizunguzungu
    Kuishiwa nguvu,kutokwa maji mengi ukeni ujue chupa imepasuka wahi hospital
    Kuwashwa ukeni na kutokwa maji maji ya njano au meupe yenye harufu wahi hospital itakuwa infection,UTI au fungus
    Pressure kupanda au kushuka,mwili kubadili rangi mikononi,miguuni,kucha n.k wahi hospital
    Kutokwa damu nyingi,mtoto kuto kucheza.

Artikel Terkait