Nafasi Ya Kazi Ya Udereva Simba Logistics Ltd Dar es salaam

Simba Logistics Ltd was established in 2008 and boasts a total fleet size of 150 vehicles and serves the Central and Dar es Salaam Corridors.  Our transport fleet includes flatbeds, drawbars, and low beds.  Most of the tractor heads in the fleet are HOWO SINOTRUK 6×4 coupled with 4 Axle Simba Trailer Drawbar Units. Our main transport destinations are the Democratic Republic of Congo (DRC), Rwanda, Burundi, Zambia and Malawi.  We have our head offices in Dar es Salaam, Tanzania.

75 Drives Jobs at Simba Logistics Ltd May, 2020

 Kampuni ya usafirishaji ya Simba Logistics Limited inawatangazia nafasi za kazi kwa madereva wa Malori. 

NAFASI: 75 Sifa za Mwombaji:
Awe amehitimu na kutunukiwa cheti halali cha Kidato cha nne au cha sita. ( mwenye vigezo zaidi atapewa kipaumbele)
Leseni halali ya Daraja E ambayo haijaisha muda wake.
Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
Awe amehudhuria mafunzo ya uendeshaji malori ya mizigo (HDV/HGV Professional Driving) kutoka Chuo cha NIT.
Waombaji wenye cheti cha majaribio ya Ufundi Daraja la II watafikiriwa kwanza.
Awe na uzoefu wa kuendesha malori ya aina zote (pulling, semi trella, intersemi, interlink n.k)

Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.

Awe na hati halali ya kitabu ya kusafiria (Passport Mpya ya Ki-electroniki).
Cheti cha kutokua na makosa yoyote ya jinai toka polisi (Police Clearance Certificate)
Kadi ya chanjo ya homa (Vaccination Card)
Awe na namba ya simu yenye mawasiliano ya whatsapp muda wote na yenye uwezo wa kupiga picha nzuri.
Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri kati ya miaka 30-45

Aambatanishe cheti cha utumishi kutoka kwa Mwajiri wa Mwisho

Jinsi ya Kutuma
Tuma Barua ya maombi iliyoandikwa kwa mkono na iambatanishwe na picha ya mwombaji Maombi yaambatane na barua ya utambulisho wa serikali za mtaa Barua ya maombi iambatane na nakala ya vyeti vya taaluma na viambata tajwa hapojuu Nakala ya cheti cha kuzaliwa au kitambulisho cha Uraia Maombi yote yawasilishwe kwa PDF kupitia email
julia@simba-logistics.com

nakala kwa Michael@simba-logistics.com

au yaletwe kwa mkono katika ofisi zetu zilizopo Tabata Matumbi,
Plot 1000,
Nelson Mandela Road,
Dar es Salaam.

Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 28 Mwezi Mei 2020 saa 10

Jioni Kwa maelezo zaidi wasiliana na Namba: 0714- 592743.