Saturday, 7 November 2020

Nafasi Mbalimbali Za Kazi Kutoka Kampuni Ya Lodhia Group


 NAFASI ZA KAZI KATI" KIWANDA KIKUBWA CHA CHUMA NA PLASTIKI
Kiwanda cha Lodhia cha Chuma na Plastiki, kilichopo kisemvule Mkuranga kinakaribisha maombi
ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa katika nafasi zifuatazo. Hii ni fursa ya kipekee kwa
Vijana wenye ndoto ya kufanya kazi na kupata ujuzi sahihi wa uendeshaji mitambo ya kisasa
katika viwanda vya chuma.

MHANDISI UMEME NA MITAMBO
(WALIOHITIMU MWAKA HUU)-NAFASI NNE

• Wahitimu wa uhandisi wenye shahada ya
kwanza na kuendelea
• Ufaulu mzuri wa masomo ya uhandisi
• Awe na ujuzi imara katika Umeme,
Mawasiliano na PLC
• Uwezo wa hali ya juu wa mawasiliano.
• Sharti awe tayari kufanya kazi zamu ya usiku
na mchana

MHANDISI WA UMEME NA MITAMBO (AWE
NA UZOEFU)-NAFASI TATU

• Wahitimu wa uhandisi wa Umeme wenye
kiwango cha chini cha shahada ya kwanza
• Ufaulu mzuri wa masomo ya uhandisi
• Uzoefu wa miaka 3 mpaka 5 kazini.
• Uzoefu wa moja kwa moja katika shughuli za
uzalishaji kwenye viwanda vikubwa. (Uzoefu
katika viwanda vya chuma ni faida kwa
muombaji)
• Sharti awe na utayari wa kufanya kazi zamu
ya mchana au usiku
• Uzoefu katika vifaa vya umeme vya kisasa,
Mawasiliano na PLC

MHANDISI WA UMEME (AWE NA
UZOEFU)-NAFASI TATU

• Wahitimu wa uhandisi umeme wenye ya
shahada ya kwanza na kuendelea
• Ufaulu mzuri wa masomo ya uhandisi
• Uzoefu zaidi ya miaka 5 katika kazi za
Umeme mkubwa, uwekaji transifoma, VCB,
njia za kusambaza Umeme na kadhalika.
• Uwezo wa kuweka kebo na HT, Laini za
umeme za LT, Usambazaji wa Umeme kutoka
kwenye transifoma kwenda kwenye kitua
cha usambazaji kiwandani.
• Ujuzi wa kutengeneza mitambo ya DC na AC
• Uwezo wa Kuweka makadirio ya kebo za
Umeme za kiwandani
• Uzoefu wa kufanyia kazi umeme wa
viwandani. (Ikiwa ni viwanda vya chuma ni
bora kwa muombaji)
• Sharti awe tayari kufanya kazi zamu ya usiku
na mchana

MHANDISI MITAMBO (WALIOHITIMU
MWAKA HUU)-NAFASI NNE

• Wahitimu wa uhandisi mitambo awe na
shahada ya kwanza ya uhandisi na
kuendelea
• Awe na msingi mzuri wa kielimu
• Ujuzi wa mitambo maji maji, Nyumatiki,
Ubadilishaji gia,
Gia boksi, beringi na kadhalika
• Sharti awe tayari kufanya kazi zamu ya
mchana na usiku

MHANDISI MITAMBO MPANGILIO NA
UENDESHAJI -
NAFASI TATU (UZOEFU WA UENDESHAJI
MITAMBO YA CNC)

• Awe na stashahada ya uhandisi mitambo
• Awe na msingi mzuri kielimu
• Uzoefu wa miaka 2-3 (Katika viwanda vya
chuma)
• Awe na uwezo wa kupangilia kituo
mbadilisho cha CNC
• Awe na uwezo wa kuendesha mashine za
CNC zinazotumika viwanda vya chuma.
• Sharti awe tayari kufanya kazi kwa zamu
mchana na usiku.

MHANDISI MITAMBO (WAHANDISI
MZOEFU DARAJA LA JUU)-NAFASI MBILI

• Mhitimu uhandisi mwenye shahada ya
kwanza au Zaidi
• Awe na msingi mzuri kielimu
• Uzoefu wa zaidi ya miaka mitano (5) kwenye
kiwanda chochote kikubwa cha uzalishaji
(Viwanda vya chuma ni bora zaidi)
• Uzoefu wa kadi ya kiotomatiki. Lazima awe
na ujuzi mzuri katika ubunifu na uwezo wa
kuelewa michoro ya kiuhandisi.
• Lazima awe na uwezo wa kubuni michoro ya
sehemu/shughuli yoyote ya kiuhandisi
mitambo.
• Ujuzi wa mitambo maji maji, Nyumatiki,
Ubadilishaji gia , Gia boksi, beringi na
kadhalika
• Lazima awe na Uzoefu wa kiutendaji kwa
vitendo.
• Sharti awe tayari kufanya kazi kwa zamu
mchana na usiku

SIFA ZA JUMLA KWA WOTE:
• Muombaji awe Mtanzania
• Muda wa mafunzo kwa vitendo
hautahesabika kama Uzoefu
• Muaminifu
• Mchapa kazi
• Anayefundishika haraka
• Mtizamo chanya wa mambo

NAMNA YA KUTUMA MAOMBI:
Tuma CV, barua ya nafasi unayomba, vyeti
vyako vya Elimu kwa anuani ya barua pepe
ifuatayo.
info-dar@lodhiagroup.co.tz
Au
Tuma CV, Barua ya nafasi unayoomba, vyeti
vyako kwa anuani ya Lodhia Steel Industries
Ltd S.L.P 75778, Dar es Salaam-Tanzania.

ZINGATIA:
Ukitumia barua pepe usitume tena kwa
sanduku la posta. Endapo utatuma kwa barua
pepe na Sanduku la barua maombi yako
hayatashulikiwa.

MUHIMU:
Kichwa cha habari cha barua pepe kisomeke
nafasi unayomba kwa usahihi bila kukosea
Mfano. MHANDISI UMEME NA MITAMBO
(WALIOHITIMU MWAKA HUU).
MWISHO WA KUTUMA:
Tutapokea maombi ya kazi mwisho tarehe
1 5/1 1/2020.

ZINGATIA:
Tutawasiliana na waombaji watakaotimiza
vigezo vya nafasi anayoomba na watakaofua
ta maelekezo ya kuomba nafasi husika kwa
usahihi. Hii ni sifa kuu ya kwanza kufuata
maelekezo kwa usahihi.

Interested candidates should send CVs and application letters to info-dar@lodhiagroup.co.tz

The deadline for submitting the application is 15 November 2020

Related Posts